bango

bango
---YOU ARE ALL WELCOME TO THE "CITY STAR BOUTIQUE" SATISFACTION GUARANTEED-OPENING HOURS FROM 9AM TO 9PM--

NEW ARRIVALS AT CITY STAR BOUTIQUE

NEW ARRIVALS AT CITY STAR BOUTIQUE

Thursday, April 19, 2012

DIAMOND ASEMA THAAAAAANX

MSHINDI wa tuzo tatu za muziki za Kili mwaka 2012 Nassib Abdul ‘Diamond’ amewashukuru mashabiki wa muziki huo kutokana na kumuwezesha kutwaa tuzo hizo. Katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaa wiki iliyopita Diamond aliongoza wasanii wenzake baada ya kutwaa tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume, Video Bora ya Mwaka kupitia wimbo wake wa Moyo Wangu na Video Bora ya Mwaka Akizungumza na mamapipiro blog juzi, Diamond alisema hana budi kuwashukuru mashabiki kwani bila wao asingeweza kutwaa tuzo hizo, hivyo amewaomba kuendelea kumpa sapoti. “Nawashukuru sana mashabiki wote na wasio mashabiki wangu kwa kuniwezesha kutwaa tuzo kwani bila nyinyi mimi si lolote, sina cha kuwalipa ila nitaendelea kuwapa kazi zilizo nzuri zaidi,”alisema. Diamond aliongeza kuwa tuzo hizo zimezidi kumpa faraja katika harakati zake za muziki kwani baada ya mwaka jana kuambulia patupu katika tuzo hizo hakukata tamaa na hivyo kuendelea kutayarisha kazi bora. Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kupata tuzo tatu kwa mpigo ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2012 alipotwaa idadi hiyo katika Tuzo za Kili pia.

1 comment: