bango

bango
---YOU ARE ALL WELCOME TO THE "CITY STAR BOUTIQUE" SATISFACTION GUARANTEED-OPENING HOURS FROM 9AM TO 9PM--

NEW ARRIVALS AT CITY STAR BOUTIQUE

NEW ARRIVALS AT CITY STAR BOUTIQUE

Tuesday, April 17, 2012

ZIARA YA WASHINDI TUZO ZA KILI 2012Diamond aliyechukua tuzo tatu, akiwa na meneja wa Kilimanjaro Beer, George Kavishe
WASANII walioshinda tuzo za muziki za Kili mwaka 2012 pamoja na wale waliokuwa wakiwania tuzo hizo wanatarajiwa kufanya ziara maalum katika mikoa sita ili kutoa shukrani kwa mashabiki sambamba na kuwapa burudani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana meneja wa bia ya Kilimanjaro inayozalishwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) George Kavishe alisema kwamba lengo la ziara hiyo pia ni kuwapa fursa mashabiki wa sehemu husika kuwashuhudia wasanii hao kwa njia ya burudani.
Alisema katika mikoa ambayo wasanii hao watapita kutaendeshwa zoezi la kuwapata wasanii chipukizi ambapo kila mkoa utatoa msanii mmoja ambaye baadaye atakuja jijini Dar es Salaam kurekodi na mmoja ya wasanii maarufu.
“Kama mnavyojua bia yetu ya Kilimanjaro ina lengo la kuwaleta watu pamoja hivyo tumeona tutumie wasanii walioshinda na wale walioshiriki kuwania tuzo kusaidia kuwapa wasanii kutoka mikoani ili kuwawezesha kufikia mafanikio kama yao,”Alisema Kavishe.
Alisema mchakato wa kuwapata wasanii hao chipukizi utaendeshwa katika tarehe maalum zilizopangwa katika kila mkoa husika huku majaji wakitarajiwa kuwa wasanii wa muziki wa bongo fleva wakiwemo Profesa J, Juma Nature na Queen Darleen.
Kavishe aliongeza kuwa ziara hiyo inatarajiwa kuanza Aprili 28 mkoani Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri, wakati Mei 7 itakuwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Kilimanjaro itakuwa Mei 12 kwenye Uwanja wa Ushirika na  Mbeya itakuwa Mei 19 katika Uwanja wa Sokoine.
Aidha wakazi wa Mtwara watapata fursa hiyo  Mei 26  katika uwanja wa Mtwara kabla ya ziara hiyo kuhitimishwa Juni 2 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar Salaam.
Baadhi ya wasanii watakaoshiriki katia ziara hizo ni pamoja na Diamond, Isha Mashauzi, Ali Kiba, At, bendi ya Twanga Pepeta, Ben Pol, Kalidjo Kitokololo, Ommy Dimples, Khadija Kopa, Suma Lee, Jaguar, Barnaba, Warriours from the East, Queen Darlin na wengineo.
Kwa upande wake msanii aliyefanikiwa kutwaa tuzo tatu mwaka huu Nassib Abdul ‘Diamond’ akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake pamoja na kushukuru kwa mashabuiki kumuwezesha kutwaa tuzo hizo, aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo watapita kufanya maonyesho.

1 comment:

  1. I admire you post . So much thanks for shared this .

    ReplyDelete